OPEN CALL FOR GENERAL MEMBERSHIP

Nafasi Art Space is a Non-profit making Contemporary Art Centre in Tanzania that provides a platform for artists through creating a centre of excellence that promotes the creativity and professionalism of Tanzanian contemporary artists, through training, exposure and cross cultural dialogue and collaborative artistic endeavours.

In line with its 2021 – 2026 strategic plan, one of Nafasi’s major objectives is to facilitate artistic development for the safeguarding of the future of artistic creation. This includes connecting artists with opportunities and resources, including accessible and inclusive membership and working space, and to professionalize their art practices and make a living through art.

The Membership programme at Nafasi offers use of Nafasi facilities (library/resource room, exhibition hall, performance stage, etc), the opportunity to take part in Nafasi organized events (trainings, workshops), access to working spaces, and opportunities for art exchange programmes within East Africa and beyond.

Nafasi is pleased to announce its open call for general memberships HERE. This is open to art students, artists of all fields and art practitioners who can work in a common shared space. The deadline for this open call is 7th May 2023.

MEMBERSHIP SUBSCRIPTION 

The Nafasi Membership programme is divided in different categories. A General Membership subscription is payable at TZS 25,000/= bimonthly OR at TZS 150,000/= annually.

The Membership subscription will be paid on a biannual/yearly basis. A new member is required to subscribe for the first year in full. The Membership  Subscription once paid will be non refundable. Failure to submit the Membership subscription within 14 days of it becoming due will result in automatic suspension of membership until the payment is made. The  Membership subscription is subject to review and amendment and may be  changed with further notice to the members.

MEMBERSHIP BENEFITS

The Membership shall give the Member Artist the right to work at Nafasi, use the  Nafasi facilities (library/resource room, work hall), take part in Nafasi organized  events, trainings and workshops. All benefits include:

  • Opportunity to become a full general member after a year of full payment and active participation
  • Opportunities for networking, exchange and participation in Nafasi’s active artistic community
  • Use of general spaces, including shared rehearsal space and meeting spaces during Nafasi’s official working hours (9am-5pm, Mon-Fri)
  • Being invited to member-only/community events at Nafasi
  • Subsidized prices on rentals
  • Support on open studios (public exhibition)
  • Member recognition on our digital platforms (Website)
  • Priority participation in trainings, workshops, and international collaborations and group exhibitions
  • Special rates on paid workshops and other training opportunities
  • Deducted commissions on selected exhibitions (for visual artists)
  • Inclusion on the Nafasi online directory
  • Opportunity for your artwork(s) to be featured on the Nafasi monthly newsletter and annual calendar
  • Access to information and opportunities within and outside Nafasi through the Nafasi community page
  • Opportunities to facilitate paid art workshops/trainings
  • Invitation to be a part of the Annual General Meeting and its privileges, such as selecting board members and approving annual budgets and plans (for active  members only)
  • Assisted promotion on selected projects/programmes for active members

For any queries, please contact us on phone number: + 255 757 820 426 or via email on: visualarts@nafasiartspace.org

APPLY HERE TO BECOME A GENERAL MEMBER


Nafasi Art Space ni Kituo cha Sanaa cha Kisasa kinachofanya kazi kwa njia isiyo ya faida nchini Tanzania ambacho hutoa nafasi kwa wasanii kwa kuunda kituo chenye ubora ambacho kinakuza ubunifu na weledi wa wasanii wa Tanzania, kupitia mafunzo, fursa na mazungumzo ya kitamaduni na juhudi shirikishi za kisanii.

Sambamba na mpango wake wa kimkakati wa 2021 – 2026, mojawapo ya malengo makuu ya Nafasi ni kuwezesha maendeleo ya kisanii kwa ajili ya kulinda mustakabali wa ubunifu wa kisanii. Hii ni pamoja na kuunganisha wasanii na fursa na nyenzo, ikijumuisha uanachama na kutoa nafasi jumuishi ya kufanyia kazi, na kuweka taaluma zao kitaalamu ili waweze kujikimu kupitia sanaa.

Programu ya Uanachama wa Nafasi Art Space inatoa matumizi ya vifaa vya Nafasi (maktaba/chumba cha rasilimali, ukumbi wa maonyesho, jukwaa la maonyesho, n.k), fursa ya kushiriki katika hafla zilizoandaliwa za Nafasi (mafunzo, warsha), upatikanajiufikiaji wa maeneo ya kufanyia kazi, na fursa za programu za kubadilishana kisanaa ndani ya Afrika Mashariki na kwingineko.

Nafasi inafuraha kutangaza wito kwa wanachama  HAPA. Hii ni fursa kwa wanafunzi wa sanaa, wasanii wa nyanja zote na wataalamu wa sanaa ambao wanapenda kufanya kazi katika jumuiya ya pamoja. Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ni tarehe 7 Mei 2023.

USAJILI WA UANACHAMA

Uanachama wa Nafasi umegawanywa katika vitengo tofauti. Usajili wa Uanachama wa Jumla unalipwa TZS 25,000/= kila baada ya miezi miwili AU kwa TZS 150,000/= kila mwaka.

Usajili wa Uanachama utalipwa mara mbili kwa mwaka/kila mwaka. Mwanachama mpya anahitajika kujisajili kikamilifu kwa mwaka wa kwanza. Usajili wa Uanachama ukishalipwa hautarejeshwa. Kukosa kuwasilisha usajili wa Uanachama ndani ya siku 14 baada ya kudaiwa kutasababisha kusimamishwa kwa uanachama hadi pale malipo yatakapofanyika. Usajili wa Uanachama unaweza kukaguliwa na kurekebishwa na unaweza kubadilishwa bila taarifa zaidi kwa wanachama.

FAIDA ZA UANACHAMA

Uanachama utampa Msanii Mwanachama haki ya kufanya kazi Nafasi, kutumia maeneo ya umma yaliyoandaliwa na Nafasi (maktaba/chumba cha rasilimali, ukumbi wa kazi), kushiriki katika hafla zilizoandaliwa za Nafasi, mafunzo pamoja na warsha. Faida zote ni pamoja na:

  • Fursa ya kuwa mwanachama mkuu kamili baada ya mwaka mmoja wa malipo kamili na kushiriki kikamilifu.
  • Fursa za kuunganisha, kubadilishana na kushiriki katika jumuiya ya kisanii ya Nafasi
  • Matumizi ya nafasi za umma, ikijumuisha eneo la pamoja la kufanyia mazoezi na maeneo ya mikutano wakati wa saa rasmi za kazi za Nafasi (3 Asubuhi- 11 jioni, Jumatatu-Ijumaa)
  • Kualikwa kwa hafla za wanachama pekee/jamii pale Nafasi
  • Kupunguziwa bei za ruzuku kwa ukodishaji
  • Usaidizi kwenye open studio (maonyesho ya umma)
  • Utambuzi wa wanachama kwenye mifumo yetu ya kidijitali (Tovuti)
  • Ushiriki wa kipaumbele katika mafunzo, warsha, na ushirikiano wa kimataifa na maonyesho ya vikundi
  • Viwango maalum pungufu kwa warsha zinazolipwa na fursa nyingine za mafunzo
  • Punguzo maalum za kamisheni kwenye maonyesho.
  • Kujumuishwa kwenye saraka (orodha ya kumbukumbu) ya mtandao ya Nafasi
  • Fursa ya kazi zako za sanaa kuonyeshwa kwenye jarida la kila mwezi la Nafasi na kalenda ya mwaka
  • Upatikanaji wa taarifa na fursa ndani na nje ya Nafasi kupitia ukurasa wa jumuiya ya Nafasi
  • Fursa za kuongoza warsha/mafunzo ya sanaa yenye malipo
  • Mwaliko wa kuwa sehemu ya Mkutano Mkuu wa Mwaka na marupurupu yake, kama vile kuchagua wajumbe wa bodi na kuidhinisha bajeti na mipango ya kila mwaka (kwa wanachama hai pekee)
  • Kusaidiwa utangangazaji wa miradi/programu za wanachama kwenye mitandao yetu (kwa wanachama wanaoshiriki kikamilifu)

Kwa maswali yoyote, tafadhali wasiliana nasi kwa nambari ya simu: + 255 757 820 426 au kupitia barua pepe kwa: visualarts@nafasiartspace.org

 

TUMA MAOMBI HAPA KUWA MWANACHAMA WETU